Ushiriki wa Kiraia

Kujitolea ni aina muhimu ya ushiriki wa raia. Pichani ni watu wa kujitolea wakifanya usafi baada ya Kimbunga Sandy cha 2012.

Ushiriki wa kiraia ni kitendo kinachohusisha mtu binafsi au kikundi cha watu katika kushughulikia mambo yanayohusu jamii. Ushiriki wa kiraia unahusisha jamii zinazofanya kazi kwa pamoja au mtu binafsi anaefanya shughuli za kisiasa na zisizo za kisiasa kwa lengo la kulinda maadili  ya umma au kuleta mabadiliko katika jamii.Lengo la ushiriki wa kiraia ni kuwasilisha matakwa ya jamii nakulinda usawa katika jamii.[1]

Ushiriki wa kiraia ni kitendo kinachohusisha watu kufanya kazi kwa pamoja ili kulinda matakwa au mahitaji ya jamii "kazi kwa ajili ya demokrasia " (Checkoway & Aldana, 2012). Chini ya uwakilishi wa vikundi vya watu wachache, watu wenye kipato cha chini na vikundi vya vijana. Kwa upande mwingine, masuala yenye vikundi vya watu wenye ushawishi mkubwa yanawasilishwa kwa haraka ili kutatua matatizo yanayoikumba jamii hiyo.(Griffin & Newman, 2008). [2]

  1. "ushiriki wa kiraia". www.apa.org.
  2. Checkoway, B., & Aldana, A. (2013). Four forms of youth civic engagement for diverse democracy. Children and Youth Services Review, 35(11), 1894–1899.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne